Picha zinazofata hapo chini ni
kutoka kwenye video fupi ambayo ilitangulizwa kama teaser ya video
kamili ya single ya ‘baadae’ ya Ommy Dimpoz.
Tuesday, 21 August 2012
Friday, 3 August 2012
KUNA WATU WANA ROHO ZA KIKATILI,EMBU SOMA STORY YA MTOTO HUYU,DEAR GOD HAVE MERCY
Mtoto
huyu anaitwa Joshua ana afya,nguvu na furaha kila wakati.Akiwa
anatambaa mama yake alimtupa huko Mbezi beach na yeye kuokotwa na mama
msamaria mwema.Mama msamaria mwema akiwa anaamka alfajiri akasikia mtoto
analia sana nje ya nyumba yake.Kwanza aliogopa sana lakini baada ya
kusikiliza kwa makini akajua ni mtoto kweli.Akatoka nje na kumkuta mtoto
kajaa tope anabiringita chini peke yake akitambaa kang'atwa na mbu
mpaka basi.
Akamchukua
na kuaanza kuita majirani kuulizana mtoto wa nani?wakaenda mpaka kwa
mjumbe,polisi,mpaka siku inaisha mama wa mtoto hakujitokeza.Basi mama
huyo akasema yeye atamchukua mtoto na kumlea kama wa kwake kabisa.Na
siku hiyo hiyo akampa jina la JOSHUA.Hivi sasa amekuwa mkubwa kwa
kumkadiria ana mwaka na miezi kadhaaa.Anamuita mama msamaria mwema
'mama' akijua huyu ni mama yake.
Mama aliyemuokota ana watoto
watatu wakubwa kabisa na Joshua ni kama kitinda mimba wake.Anampenda
sana huyu mtoto na anamlea kwa mapenzi yote ya mama kwa mtoto.Anasema
amehifadhi zile nguo alizomuokota nazo ili akija kuwa mkubwa amwambie
ukweli na kumuonyesha zile nguo.Anajua itakuwa ngumu kumueleza ukweli
hapo baadae ila itabidi tu amwambie ili ajue.
Nimejaribu kutafakari amekuwa mkubwa halafu mama aliyemlea na yeye kujua ni mama yake mzazi ana mwambia kuwa alimuokota.Atajisikiaje?itamuumaje?
Nimejaribu kutafakari amekuwa mkubwa halafu mama aliyemlea na yeye kujua ni mama yake mzazi ana mwambia kuwa alimuokota.Atajisikiaje?itamuumaje?
Hii story nimeitoa kwa Dinamarios.blogspot.com kama ilivo,So touching Mungu Amzidishie mama alie okota Mtoto huyu.
Subscribe to:
Posts (Atom)