NZI motomoto kati ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul
‘Diamond’ na Mrembo Nambari 3 wa Tanzania 2006, Jokate Mwegelo limedaiwa
kuvunjika, Risasi Jumamosi linatambaa nayo.
Kwa mujibu wa chanzo
chetu, raia wa Tanzania anayecheza mpira wa kikapu nchini Marekani,
Hasheem Thabit Manka anatajwa kuwa chanzo cha penzi la wawili hao
kusambaratika.
KWA NINI?
Awali, Thabit aliwahi kuripotiwa na
baadhi ya vyombo vya habari kwamba ‘anatoka’ na Jokate, madai ambayo kwa
upande wake mrembo huyo aliyakanusha vikali akisema anasingizwa licha
ya kujikanyaga katika maelezo yake.
Hata hivyo, baadaye wawili hao
ikasemekana wamemwagana kwa sababu ambazo hazikuwa wazi kwa vile
uhusiano wao ulikuwa wa siri kubwa.
WAMERUDIANA?
Safari hii, kwa mujibu wa chanzo
chetu, Hasheem amemrudia Jokate kwa nguvu zote huku ikidaiwa kwamba
hitimisho la uhusiano wao litaishia kwenye kufunga ndoa na kuishi kama
mke na mume.
KUMWAGANA KWA DIAMOND NA JOKATE
Sosi mmoja
alimjulisha paparazi wetu kwa staili ya kumuuliza swali kama anafahamu
lolote kuhusu wapenzi hao kupeana mkono wa kwaheri.
“Hivi jamani
mnajua kama Jokate na Diamond wamemwagana? Demu amerudiana na Hasheem
Thabit, tena safari hii watafunga ndoa kabisa,” alisema sosi huyo.
Akazidi
kudai kuwa mbaya zaidi, Jokate amekata waya wa mawasiliano kati yake na
Diamond, hali ambayo inampa wakati mgumu jamaa kwani uhusiano wao
umevunjika huku akiwa bado anampenda.
‘WATUHUMIWA’ WASAKWA
Ili kupata uhakika wa madai
haya, Risasi Jumamosi lilimsaka Diamond kwa njia ya simu ambapo
alipopatikana na kuulizwa kuhusu madai hayo, alikuwa na haya ya kusema:
“Hamna,
hamna kitu kama hicho. Unajua mambo kama hayo msiandike. Mimi
nitaondoka keshokutwa kwenda kufanya shoo Big Brother, si umesikia?”
Paparazi:
Yeah! Tumesikia, habari tayari ipo kwenye gazeti.
Diamond: Basi
ndiyo hivyo, hiyo habari ya Jokate bwana hamna kabisa.
JOKATE
NAYE ASOMEWA MASHITAKA
Baada ya kuongea na Diamond, paparazi wetu
alimtwangia simu Jokate ambapo alisikiliza madai mwanzo hadi mwisho
lakini badala ya kujitetea au kufafanua, alikata simu.
WEMA ATOA LA MOYONI
Kwa upande wake, aliyekuwa
mchumba wa Diamond, Wema Sepetu alipoulizwa kuhusu kuvunjika kwa
uhusiano wa wawili hao, alisema:
“Nilisema mimi mkanipuuza, sasa
mmekiona alichokifanya Jokate? Naamini ni laana yangu kwani mimi
sikuwahi kumfanyia jambo lolote baya Diamond. Mungu ameona, amenilipia.
Teh! Teh! Teh!”
TUJIKUMBUSHE
Awali, ukiachana na mademu wengine,
Diamond aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema. Penzi lao
lilifikia hatua nzuri kwa mwanaume huyo kumvisha pete ya uchumba mrembo
wake huyo.
Hata hivyo, uchumba wao ulivunjika baadaye huku Wema
akimshutumu Jokate kwamba ndiye chanzo.
Jokate mwenyewe amekuwa
akikana kuwa na uhusiano na Diamond lakini ilifika mahali mambo yakawa
hadharani, Diamond akakiri kweupe kuwa anampenda sana mlimbwende huyo na
hakuna anayeweza kuvuruga uhusiano wao.
Siku za karibuni, kuliibuka
madai kwamba mcheza filamu mwenye heshima nusunusu Bongo, Aunt Ezekiel
na Diamond walinaswa wakiwa kwenye hoteli moja jijini Dar es Salaam,
hali iliyodaiwa kumfanya Jokate kulia wivu kwa kitendo hicho.
Kwa
maana hiyo, kama Jokate amerudiana na Hasheem inawezekana kitendo cha
Diamond kudaiwa kukutwa na Aunt kimechangia.