Wataalamu kutoka China wameanza kutoa huduma ya kunyanyua maziwa ya mwanamke kwa kutumia mashine maalumu ambapo hiyo huduma imeanza kusimamisha maziwa yaliyolala, imeanza kutolewa katika Saluni moja Sinza jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu kutoka China aitwaye, Ciisy Pang, ni binti wa miaka 23 tu, lakini anasema kwa miaka minne amefanya kazi hiyo na kuwasaidia wanawake mbalimbali waliokuwa wakikerwa na matiti yaliyolegea au kuanguka.
Pang na kundi lake wanatoa huduma hii kwa gharama ya Sh150,000 kwa kuanzia, ingawa wanahisi gharama hizo zitapanda katika siku chache zijazo.
Mashine wanayoitumia inaitwa ‘Beauty Machine’ ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila saizi kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli ambapo kazi yake kubwa ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti ambapo pia zoezi la kusimamisha matiti huchukua wiki tatu mpaka sita, inategemea aina ya mteja na wakati mwingine juhudi zake.
Kingine ni kwamba hawatumii dawa yoyote katika hilo zoezi, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama zilivyo dryer za nywele, wanaiwasha kwa muda wa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya hilo zoezi mpaka litakapokamilika,
Tangu mashine hiyo imeletwa bongo mwezi mmoja uliopita, Pang anasema ana wateja nane anaowahudumia kwa muda tofauti ambao wamekiri kuwa maendeleo yanatia moyo
na mie nazisaka niendee nikakazie.........
No comments:
Post a Comment