China ni moja ya nchi zizotusaidia sana,tuwashukuru kwa hilo........
Naibu
Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (kulia ) akisaini kitabu cha
wageni cha Wizara ya Fedha jijini Dar es salaam wakati
alipokwenda kusaini mkopo na misaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu
wa China kwa ajili ya kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali
inayozidi shilingi bilioni 80. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri wa
Fedha Mustafa Mkulo(hayupo pichani) kwa niaba ya Tanzania na Naibu
Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao.
Waziri
wa Fedha Mustafa Mkulo(aliyesimama ) akitoa hotuba jijini Dar es salaam
wakati wa sherehe fupi ya kusaini mkopo na misaada kutoka Serikali ya
Jamhuri ya Watu wa China. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri Mkulo kwa
niaba ya Tanzania na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (hayupo
pichani) . Msaada na Mkopo huo unazidi bilioni 80 Fedha za Kitanzania.
Kushoto ni Waziri wa Uchukuzi Omar Nundu na kulia ni Waziri wa Nishati
na Madini William Ngeleja.
Waziri
wa Fedha Mustafa Mkulo(kushoto) na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li
Jinzao (kulia) wakisaini makubaliano jijini Dar es salaam ya Serikali
ya China kuipa mkopo nafuu na msaada kwa ajili ya shughuli mbalimbali za
maendeleo nchini. Msaada na mikopo hiyo ni zaidi bilioni 80 fedha za
Kitanzania ambayo inazidi kuimarisha urafiki na undugu kati ya Tanzania
na China.
Naibu
Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (aliyesimama ) akitoa hotuba
jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kusaini mkopo na misaada
kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya kuisaidia
Tanzania. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo
(hayupo pichani) kwa niaba ya Tanzania na Naibu Waziri wa Biashara wa
China Li Jinzao. Kulia ni Balozi wa China nchini Lu Youqing.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliackim Chacha(katikati)
akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia
Dkt. Florence Turuka(kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi
Mhandisi Omar Chambo jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya
kusaini makubaliano kati ya Serikali ya China na Tanzania ya kuipa mkopo
nafuu na msaada kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ambao
ni zaidi bilioni 80 fedha za Kitanzania.(habari na mo-blog)
No comments:
Post a Comment