Afande na 20%wakionekana wamejeruhiwa na kichapo cha polisi
Baada ya wasanii 20% na Afande Sele kuachiwa kwa dhamana huko Morogoto 88.5, Afande Sele kwa kujiamini ametoa kauli nzito kwa ajili ya polisi wa Morogoro.
Baada ya kuachiwa huru baada ya kupigwa sana mikononi mwa polisi, Afande Amesema “katika rekodi yangu ya maisha sijawahi kuwa na shida yoyote na polisi sio Morogoro tu lakini wanavyoiendesha polisi sasa hivi sio polisi wa Morogoro tuliowazoea, hivi ni vipolisi flani mchanganyiko na Mgambo vimetoka huko vimeshaharibu vimekuja hapa kuzingua watu, ndio wala rushwa wakubwa ndio wanaotumika vibaya ila sina ugomvi nao”
Afande ameamplfy zaidi kwamba “ugomvi wao mkubwa wanatumwa kwa sababu wanajua Afande atagombania ubunge kwa hiyo ni chuki tu ila ubunge ni sehemu ya maisha yangu”
Amesema chanzo cha hayo yote ni mwizi alieiba pikipiki yao ambapo mdogo wake Afande ndio alikwenda kumkamata ila kwa sababu polisi walikua wameshapewa rushwa wakaamua wamuachie mwizi wamkamate mdogo wake, wakawakamata na gari yangu bila sababu.
Afande amesema “baada ya hapo nikaenda kuchukua gari yangu kumbe walikua wananivizia mimi tu ikabidi waanze kupiga mabomu baada ya kuona watu wamejaa manake wametupiga sana mimi na 20% wakati tulipofata gari, wananchi waliona haiwezekani kumpiga mbunge wao mtarajiwa, mfalme wao na kila kitu chao kwa hiyo wakapigana, wakapambana sana mpaka polisi wakapiga mabomu pakageuka uwanja wa vita kwa muda mfupi, polisi wakaamua kulipa kisasi kwa kutupeleka magereza na kila sehemu toka juzi lakini tunashukuru Mahakama imetenda haki”
20% ameamplfy kwamba “tumetoka kwa dhamana kwa sababu kesi zote zinaendana yani ndani ya muda mmoja tuna kesi tano, alafu sio kweli kwamba mimi kwenye hilo tukio nilikua nimevaa chupi, hakuna mtu anaweza kukwambia mimi nilikua uchi”
April 4 2012 Polisi Morogoro walithibitisha kukamatwa na polisi kwa 20% na Afande Sele April 3 2012 ambapo kamishna mwanamizi alisema “sisi tumeshawapeleka mahakamani tayari, sio kweli kwamba walimpiga polisi ila kulikua na rafiki yao ambao walikua wamepishana lugha kwa hiyo walikua wanamtafuta na kuja kwenye eneo la benki ya NMB wakiwa wamevaa vichupi wakiwa na mapanga mkononi, watu wakataharuki mchana ule na kuizonga benk na kuvunja vioo vya magari”
Read more http://www.millardayo.com

No comments:
Post a Comment