Hatimae Waziri wa habari
Emmanuel Nchimbi kwa kushirikiana na mbunge wa Singida Mashariki Tundu
Lissu wamefanikiwa kusuluhisha mgogoro wa kimaslahi kati ya mbunge wa
mbeya mjini Joseph Mbilinyi na meneja uzalishaji vipindi CLOUDS MEDIA
GROUP Ruge Mutahaba kuhusiana na haki za wasanii wa muziki wa
bongofleva.
Waziri Nchimbi amesema
“wamekubaliana na kusaini kumaliza tofauti baada ya kufanyika kikao cha
mwisho cha upatanishi kati ya Ruge na Mr II ambapo katika upatanishi
huo, pande zote mbili ziliridhika kuwa msingi wa mgogoro wao ni kuamini
kwamba upande mmoja hauutendei haki upande mwingine”
Waziri Nchimbi amezidi kusema
kwamba “kwenye hotuba yangu kwenye bunge lililopita kuhusu vijana
Afrika, nilizungumzia haja ya watu kumaliza tofauti zao na kusameheana
ambapo baada ya kutoka kwenye mkutano ule Mh Joseph Mbilinyi alikuja
kuniona akaniambia muheshimiwa Waziri unajua umeongea mambo ya maana
lakini nilitarajia baada ya kusemea pale kwenye kipaza sauti ungekuja
kuniambia mimi, haya tuanze huo mchakato wa suluhu, nikamwambia
hatujachelewa, bado tunaweza kufanya, nikamuuliza kama ni kweli tufanye
mazungumzo ya kuwapatanisha wote wakakubali baada ya kufanya vikao vya
kutosha”
Kwa upande wake Ruge Mutahaba
amesema “tumepanga mikakati ya jinsi tutakavyokua tunakutana na Mh
Sugu kuendelea kusaidia sanaa yetu hii, ni kweli kabisa tumesaini bila
shinikizo lolote, tunaamini sasa ni hatua ya kusogea mbele tuachane na
yaliyopita”
Mr II alifunga mjadala kwa kusema kwamba “ni kweli tulikua katika vita na vita lazima ifike
mwisho labda iwe ni vita isiyo na malengo ndio haitaki suluhu lakini
kama ilikua na malengo ina maana inapopatikana fursa ya suluhu kama
kweli ulikua na dhamira a dhati kwa kile unachokipigania lazima ukubali
kukaa chini na kutafuta suluhu ili tusonge mbele, tumekubaliana, sasa
tunasonga mbele na wengine sasa hivi tupate fursa sasa hivi kujikita
zaidi kwenye siasa za kitaifa”(read more on Millardayo official website)
Wakati mwingine ugomvi uwa hausaidii,naungana nao kwa hatua waliochukua,Sugu alisisitiza kwa waliokuwa wanaunga mkono ugomvi huu nao waone kuwa sasa yameisha.
i think both are the one who push our music where we are today what we need is 4 them to fight rights of bongo fleva artist coz they ain't get anything i what they do in this industry
ReplyDeleteuko sahihi,wanamchango mkubwa sana,kugombana sio kitu kizuri
ReplyDelete