Kamati ya kudumu ya bunge ya
hesabu za serikali imeitaka wizara ya kazi na ajira kuweka utaratibu
maalum utakaowezesha wageni kutoajiriwa kwa kazi ambazo wanaweza
kuzifanya watanzania ili kulinda ajira za Watanzania.
Akizungumza kwenye kikao cha
kamati hiyo na Wizara ya kazi na ajira, Mwenyekiti wa kamati hiyo John
Cheyo amesema wakati umefika kwa Tanzania kulinda kikamilifu nafasi za
kazi zinazoweza kuwalinda watanzania wasio ajira.
Katibu mkuu wizara ya kazi na
ajira Erick Shitindi amesema kinachwakwamisha kwa sasa ni kuwepo kwa
sheria tatu ambazo zinaruhusu kituo cha uwekezaji (TIC) kutoa vibali,
uhamiaji kutoa vibali na wizara kutoa vibali hivyo pia kwa hiyo mamlaka
hayako sehemu moja peke yake.
No comments:
Post a Comment