Friday, 3 August 2012

KUNA WATU WANA ROHO ZA KIKATILI,EMBU SOMA STORY YA MTOTO HUYU,DEAR GOD HAVE MERCY

 
Mtoto huyu anaitwa Joshua ana afya,nguvu na furaha kila wakati.Akiwa anatambaa mama yake alimtupa huko Mbezi beach na yeye kuokotwa na mama msamaria mwema.Mama msamaria mwema akiwa anaamka alfajiri akasikia mtoto analia sana nje ya nyumba yake.Kwanza aliogopa sana lakini baada ya kusikiliza kwa makini akajua ni mtoto kweli.Akatoka nje na kumkuta mtoto kajaa tope anabiringita chini peke yake akitambaa kang'atwa na mbu mpaka basi.
 
Akamchukua na kuaanza kuita majirani kuulizana mtoto wa nani?wakaenda mpaka kwa mjumbe,polisi,mpaka siku inaisha mama wa mtoto hakujitokeza.Basi mama huyo akasema yeye atamchukua mtoto na kumlea kama wa kwake kabisa.Na siku hiyo hiyo akampa jina la JOSHUA.Hivi sasa amekuwa mkubwa kwa kumkadiria ana mwaka na miezi kadhaaa.Anamuita mama msamaria mwema 'mama' akijua huyu ni mama yake.
Mama aliyemuokota ana watoto watatu wakubwa kabisa na Joshua ni kama kitinda mimba wake.Anampenda sana huyu mtoto na anamlea kwa mapenzi yote ya mama kwa mtoto.Anasema amehifadhi zile nguo alizomuokota nazo ili akija kuwa mkubwa amwambie ukweli na kumuonyesha zile nguo.Anajua itakuwa ngumu kumueleza ukweli hapo baadae ila itabidi tu amwambie ili ajue.

Nimejaribu kutafakari amekuwa mkubwa halafu mama aliyemlea na yeye kujua ni mama yake mzazi ana mwambia kuwa alimuokota.Atajisikiaje?itamuumaje?
Hii story nimeitoa kwa Dinamarios.blogspot.com  kama ilivo,So touching Mungu Amzidishie mama alie okota Mtoto huyu.

No comments:

Post a Comment