Sunday, 19 June 2016

UNAITIZAMAJE DHANA YA MICHANGO YA HARUSI?

Hii dhana ya michango ya harusi naitizama tofauti kabisa,nikiwa Na maswali kibao.

Baadhi ya Watu mtakubaliana Na mim kuwa michango sasa hivi imekuwa kama Mzigo.

unaeza jikuta una michango minne ndani ya mwez mmoja bado hapo hujafikiria Zawadi unakuta wote ni watu wako Wa karibu.

Najiuliza kwa Maisha ya kawaida ya kipato cha kawaida haiwezekan kabisa kusave hela ya harusi Na kufanya harusi bila michango?

Swali lingine najiuliza wazee watu zaman walifanyaje harusi zao?Sawa inaaeza kuwa Zama hizi Na zile tofauti kuna ulazima Wa kufanya harusi kubwa sana? Why watu wasifanye harusi ya kawaida tu?kwakuwa  wengi huwa wanamaliza harusi Na madeni Yaan baada ya harusi kwisha mke Na mume wanaaanza kupambana kulipa Madeni!!!

Ni lazima kufanya harusi kubwa? Hakuna namna dhana hii inaeza kubadilishwa?Na Ndoa nyingi hazidumu miaka ya hivi karibuni.

Nimewaza Tu,We Need to change This,it has been a cultural Practice mi nahis kama inalemaza bwana harusi,maana ukiwa unategemea michango automatically utaidai ipasavyo ili ufanikiwe.Hence inafanya anaetakiwa kutoa aone kama lazima sip option.

😉😉😉😉😉😉😉

No comments:

Post a Comment