
Picha:- Waziri
 wa habari, vijana utamaduni na michezo Emmanuel Nchimbi, Mbunge wa 
Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (MR II), Meneja uzalishaji vipindi Clouds 
Media Group Ruge Mutahaba & Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
Hatimae Waziri wa habari 
Emmanuel Nchimbi kwa kushirikiana na mbunge wa Singida Mashariki Tundu 
Lissu wamefanikiwa kusuluhisha mgogoro wa kimaslahi kati ya mbunge wa 
mbeya mjini Joseph Mbilinyi na meneja uzalishaji vipindi CLOUDS MEDIA 
GROUP Ruge Mutahaba kuhusiana na haki za wasanii wa muziki wa 
bongofleva.
Waziri Nchimbi amesema 
“wamekubaliana na kusaini kumaliza tofauti baada ya kufanyika kikao cha 
mwisho cha upatanishi kati ya Ruge na Mr II ambapo katika upatanishi 
huo, pande zote mbili ziliridhika kuwa msingi wa mgogoro wao ni kuamini 
kwamba upande mmoja hauutendei haki upande mwingine”
Waziri Nchimbi amezidi kusema
 kwamba “kwenye hotuba yangu kwenye bunge lililopita kuhusu vijana 
Afrika, nilizungumzia haja ya watu kumaliza tofauti zao na kusameheana 
ambapo baada ya kutoka kwenye mkutano ule Mh Joseph Mbilinyi alikuja 
kuniona akaniambia muheshimiwa Waziri unajua umeongea mambo ya maana 
lakini nilitarajia baada ya kusemea pale kwenye kipaza sauti ungekuja 
kuniambia mimi, haya tuanze huo mchakato wa suluhu, nikamwambia 
hatujachelewa, bado tunaweza kufanya, nikamuuliza kama ni kweli tufanye 
mazungumzo ya kuwapatanisha wote wakakubali baada ya kufanya vikao vya 
kutosha”
Kwa upande wake Ruge Mutahaba 
amesema “tumepanga mikakati ya jinsi tutakavyokua tunakutana na Mh 
Sugu kuendelea kusaidia sanaa yetu hii, ni kweli kabisa tumesaini bila 
shinikizo lolote, tunaamini sasa ni hatua ya kusogea mbele tuachane na 
yaliyopita”
Mr II alifunga mjadala kwa  kusema  kwamba “ni kweli tulikua katika vita na vita lazima ifike
 mwisho labda iwe ni vita isiyo na malengo ndio haitaki suluhu lakini 
kama ilikua na malengo ina maana inapopatikana fursa ya suluhu kama 
kweli ulikua na dhamira a dhati kwa kile unachokipigania lazima ukubali 
kukaa chini na kutafuta suluhu ili tusonge mbele, tumekubaliana, sasa 
tunasonga mbele na wengine sasa hivi tupate fursa sasa hivi kujikita 
zaidi kwenye siasa za kitaifa”(read more on Millardayo official website)
Wakati mwingine ugomvi uwa hausaidii,naungana nao kwa hatua waliochukua,Sugu alisisitiza kwa waliokuwa wanaunga mkono ugomvi huu nao waone kuwa sasa yameisha.
i think both are the one who push our music where we are today what we need is 4 them to fight rights of bongo fleva artist coz they ain't get anything i what they do in this industry
ReplyDeleteuko sahihi,wanamchango mkubwa sana,kugombana sio kitu kizuri
ReplyDelete