Friday 6 April 2012

BAADA YA SHUTUMA KIBAO ZA WEMA KATIKA MEDIA KUMSHUTUM DIAMOND,PLATINUMZ AFUNGUKA KUPITIA WEBSITE YA MILLARDAYO KWA KUSEMA MENGINE MENGI NA KWAMBA HATOKUJA KURUDIANA NA WEMA KWANI YALIYOMKUTA NA KILICHOMFANYA WAACHANE NA WEMA NI N................(habari inajieleza)




Enzi za mapenzi yao(twosome)pichani wakiwa Southafrica


































Baada ya kuamua kutokaa kimya kutokana na shutuma zilizotolewa dhidi yake na mpenzi wake wa zamani WEMA SEPETU, Mwimbaji DIAMOND PLATNUMS ameamua kutoa kauli yake ya mwisho kuhusu Wema.

Diamond anakiri kwamba hakutaka kabisa kumzungumzia Wema kwenye vyombo vya habari baada ya kuachana kwa sababu hakutaka malumbano lakini imebidi iwe hivyo kwa sababu ya hasira aliyoipata kutokana na Wema kuzungumza uongo mwingi dhidi yake.

Exclusive na millardayo.com Diamond amekiri kwamba aliachana rasmi na Wema mwezi january mwaka huu na hiyo ni kutokana na kukerwa na tabia za Wema alizozikemea lakini mwisho wa siku hakufanikiwa, zikawa zinaendelea…. ambapo tabia hizo ni pamoja na Wema kuwalipa waandishi wa habari wa magazeti ili watoe stori zake, japo Diamond alikua anawalipa waandishi wasiandike chochote, yeye alikua anawalipa zaidi.

Diamond amesema “kuna vitu vya chinichini alikua ananifanyia vya kuniumiza kama kudanganyana lakini nilikua sivipeleki kwenye vyombo vya habari kwa sababu nilikua namuheshimu namfichia kwa sababu anasema hafanyi hivyo, lakini akawa anaendelea kuvifanya kama kunidanganya kwenye mapenzi japo kudanganyana kwenye mapenzi ni kitu cha kawaida hata wapenzi wangu wa zamani walikua wananidanganya na mimi nawadanganya pia, lakini alikua anapeleka kila kitu kwenye magazeti hata vitu vya watu wawili ndani ya nyumba anavipeleka, sasa nyumba inakua haina siri”
Ameamplfy zaidi kwamba “Wema alikua anapeleka stori kabisa yani kitu tumefanya watu wawili ndani unashangaa kukikuta kwenye gazeti, nikikutana na waandishi ambao ni rafiki zangu wananiambia ebwana wewe unajisumbua bure yeye mwenzako akija hapa ndio anataka aandikwe, mimi nilishawahi kumkuta hotelini uchi kabisa akiwa na mwanaume mwingine hotelini mwishoni mwa mwaka jana lakini sikuongea chochote kwenye vyombo vya habari, nikamchukua na kuondoka, niliamua kumtunzia siri yake na nikanyamaza kwa kuichukulia kama mwanaume, na hata nikawa nikifika kwenye media nilikua nampamba na kumtetea kwamba jamani Wema hayuko hivyo na ni mstaarabu”

No comments:

Post a Comment