Friday, 6 April 2012

NILIKUWA NAFUNGUA BLOG YA SHAFII DAUDA KWA LENGO LINGINE NIKAKUTA HABARI HII,NIMESIKITISHWA NA NGUVU ZIKANIISHA HAPO HAPO,RIP KANUMBA WE LOVED YOU

BREAKING NEWSSSSSSSSSSS: MUIGIZAJI STEVEN KANUMBA APATA AJALI NA KUFARIKI DUNIA

Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya wasanii wenzake wa filamu Steven Kanumba amefariki dunia usiku huu wa saa 9 kutokana na kupata ajali ambayo ilimpelekea kudondoka chini na kufikia kichwa usiku huu. Taarifa zaidi zitaendelea kukujia kila tutakapozipata. Mwenyezi mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Steven Charles Kanumba.

UPDATES: Watu tofauti kutoka kada tofauti, wakiwemo wasanii wa filamu na muziki wanazidi kufurika nyumbani kwa Kanumba hapa Sinza, simamzi imetawala kwa kiasi kikubwa watu wanalia sana. Kiukweli inasikitikitsha.


UPDATES:  Kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijadhibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.

UPDATES: Ndugu wa marehemu wakiwemo mdogo wake amethibitisha kifo cha kaka yake na kusema taarifa rasmi ya kifo chake itatolewa asubuhi.

ALIYOYAANDIKA YA MWISHO MWISHO KWENYE PAGE ZAKE ZA FACEBOOK & TWITTER

Hivi ndivyo ukurasa wake wa facebook unavyoonekana.

.

.

.

Hii ndio ilikua tweet yake ya mwisho.

1 comment: