Wednesday, 15 February 2012

SINTAH KUTAJA IDADI YA WANAUME ALIODATE NAO BAADA YA KUACHANA NA NATURE MIKA KUMI ILIYOPITA KATIKA MAHOJIANO NA MILLARD AYO


Sintah.
Wiki moja tu baada ya kutangaza mpango wa kucheza movie inayohusu maisha yake ya kimapenzi na staa wa bongo fleva JUMA NATURE walieachana miaka kumi iliyopita, Mwigizaji Sintah idadi ya wanaume aliokua nao toka aachane na Nature.

Exclusive na millardayo.com , Sintah amesema amewahi kuwa na wanaume wawili tu katika muda wote huo, na sasa yuko single.
Ameamplfy kwamba “sababu zangu kubwa za mimi kuachana na wanaume sio kufumania au kugundua ananidanganya, lakini kinachonifanya niachane nao ni tatizo kama kufatana fatana, mwanaume hajiamini kwamba mimi nimpenzi wake, kila saa anaota anaibiwa, hilo ndio tatizo kubwa lilinlonifanya niachane nao”
Amesema “mwanaume asiponijali hilo ni tatizo pia, kuhusu wivu wakati mwingine naweza kuelewa kwa sababu mimi ni Mzuri na ninajijua ila wivu usizidi”
Kwa sasa Sintah anajiandaa kuuza kwenye movie mpya atakayocheza na Juma Nature kuigiza maisha ya mapenzi yao ambayo yalidumu kwa mwaka mmoja zaidi ya miaka kumi iliyopita, movie ambayo itapatikana kwenye CD mbili tofauti, Behind the scene na movie yenyewe, ambapo Sintah amesema mchekeshaji maarufu duniani Mr Been atahusika pia, na inatarajiwa kutoka ndani ya miezi mitatu ijayo

No comments:

Post a Comment