Wednesday 15 February 2012

WIZARA YA AJIRA NA KAZI YATOA SABABU ZA KUSHINDWA KUDHIBITI AJIRA KUVAMIWA NA WAGENI!


Mfanyabiashara wa kichina akisafirisha bidhaa kwa kutumia Bajaji (picha kutoka jamii Forum).
Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali imeitaka wizara ya kazi na ajira kuweka utaratibu maalum utakaowezesha wageni kutoajiriwa kwa kazi ambazo wanaweza kuzifanya watanzania ili kulinda ajira za Watanzania.
Akizungumza  kwenye kikao cha kamati hiyo na Wizara ya kazi na ajira, Mwenyekiti wa kamati hiyo John Cheyo amesema wakati umefika kwa Tanzania kulinda kikamilifu nafasi za kazi zinazoweza kuwalinda watanzania wasio ajira.
Katibu mkuu wizara ya kazi na ajira Erick Shitindi amesema kinachwakwamisha kwa sasa ni kuwepo kwa sheria tatu ambazo zinaruhusu kituo cha uwekezaji (TIC) kutoa vibali, uhamiaji kutoa vibali na wizara kutoa vibali hivyo pia kwa hiyo mamlaka hayako sehemu moja peke yake.

hapa ni Kariakoo washkaji wakisafirisha mzigo
source:www.millardayo.com(official website)

No comments:

Post a Comment