Saturday, 11 February 2012

WEMA KANUNULIWA GARI KAMA PONGEZI BAADA YA KUACHANA NA DIAMOND,NA KAFUNGUKA ZAIDI KWAMBA JAMAA ALIKUWA ANAMPA MIKOSI SINCE KAACHANA NA JAMAA MAMBO YAKE YANAMWENDEA POA

Msanii wa filamu Bongo asiyeishiwa na matukio, Wema Sepetu amenunuliwa gari la kifahari na ndugu zake huku ikidaiwa kuwa ni pongezi kwa kuachana na mchumba wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Wema hivi karibuni aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, gari hilo la shilingi milioni 35 aina ya Toyota Lexus lenye namba za usajili T 211 BXR, amenunuliwa na mama yake pamoja na ndugu wengine kufuatia kufurahishwa na uamuzi mgumu aliouchukua.

Madai ya kuhongwa
Awali kulikuwa na tetesi kuwa, gari hilo analotumia mrembo huyo kwa sasa amehongwa na mwanaume aliyechukua nafasi ya Diamond.

kazidi kudaiwa kuwa, lengo la mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Clemence kumnunulia Wema gari ni kumwepusha na vishawishi kutoka kwa wanaume mapedeshee.
“Lile gari analotembelea Wema kanunuliwa na yule jamaa yake wa sasa, si unajua tena mtoto mzuri kama yule hawezi kutumia daladala au teksi?” kilishadadia chanzo hicho ambacho ni rafiki wa Wema.

Wema afunguka
Akizungumzia madai hayo, Wema alisema wanaoamini amehongwa gari hilo wanakosea kwani ukweli ni kwamba amenunuliwa na ndugu zake kama zawadi.
“Najua kila mmoja atakuwa na lake la kusema juu ya hili gari ninalotumia kwa sasa, ukweli ni kwamba nimenunuliwa na mama na ndugu zangu wengine baada ya kutoka kwenye kashikashi zito na Diamond.
“Na mimi zaidi ya kuwashukuru pia naahidi kutowaangusha na nitajitahidi kutowakosea kwa namna yoyote ile,” alisema Wema.

Wema alikuwa mpenzi baadaye mchumba wa Diamond lakini hivi karibuni wawili hao walitibuana huku pia kukiwa na madai kuwa baadhi ya ndugu wa Wema walikuwa hawafurahishwi na uhusiano wao.

3 comments:

 1. mmmmhhh, stil after a few mnths tutasikia jipya about this chick.

  ReplyDelete
 2. mimi nampongeza sana wema. ki ukweli niko upande wa wema kwa asilimia 100. nampenda sana huyu dada kwa vile anajua thamani ya kupendwa. na ninamuona ni kama innocent anayeangukia kwenye mapenzi na vibaka wa mapenzi. POLE SANA WEMA.binafsi namchukia sana diamond japo mziki wake naupenda sana na ni shabiki wa diamond. kijana huyu namfahamu tangu akiwa underground hajulikani hata mtaani kwake na sasa diamond celebrity anabadilisha waschana anavyopenda. umaarufu alonao umemfanya akawa mpumbavuuuuuuuuuuuuuuuuuu tena sana tu ila sio siku nyingi ataanguka na kuna wanamziki wazuri kuliko yeye wanachipukia.
  namshari sasa wema atulie kwa mda atafte mwanaume wa ukweli wa kumuoa.tena aachane na ma celebrity aolewe na watu wa kawaida tu. ningekuwa sijaoa basi mimi nilikuwa tayari kabisa kfunga ndoa na wema kwani nampenda sana.

  ReplyDelete
 3. as a simple advice to this chick,umri unakwenda you better find a man who will marry you forever!!we are sick and tired about you.

  ReplyDelete