Thursday, 16 February 2012

WANAWAKE TISA MATAJIRI AFRICA

1
.1. Wendy Appelbaum wa Afrika Kusini, ana dola za kimarekani milioni 25.3
2) Wendy Ackerman wa Afrika kusini ni mfanyabiashara, ana dola za kimarekani milioni 190.2
3) Isabel Jose Dos Santos wa Angola ana dola za kimarekani milioni 170, ni mke wa milionea wa kikongo Sindika Dokolo, na pia ni mtoto wa rais Dos santos, ana tanesco yake, benki mbili, kampuni za mafuta na biashara nyingine.Alianza biashara akiwa na umri wa  miaka 24 kwa shinikizo la baba yake.
4) Bridgette Radebe ni Msouth Afrika mwenye umri wa miaka 52, anadili na biashara ya madini.
5) Mamphela Ramphele wa Afrika Kusini, ana umri wa miaka 65, yuko kwenye biashara ya madini pia katika kampuni iliyotoa ajira za wafanyakazi elfu 45, mkwanja alionao ni dola za kimarekani milioni 90.
6) Irene Charnley wa Afrika Kusini, ana umri wa miaka 52, alishawahi kuwa director wa kampuni ya simu za mkononi ya MTN South Africa, lakini kabla alishawahi kuwa director wa FirstRand Bank na Smile Telecoms.
7) Pam Golding wa South Africa, ni mwanzilishi wa kampuni ya kuuza na kupangisha majumba ya kifahari katika kisiwa cha Mauritas na afrika kusini. Alianza biashara yake mwaka 1976, anamiliki dola za kimarekani milioni 86.
Moja kati ya nyumba zilizoko kwenye mikono ya kampuni yake.

8)  Sharon Wapnik wa Afrika Kusini, ana dola za kimarekani milioni 43.1, biashara zake ni kuuza nyumba pia na kukodisha pia, ni mwanasheria, pia mwenyekiti na Director wa Premium Properties Limited.

9) Msouth Africa Elisabeth Bradley ana dola za kimarekani milioni 32, ni mwenyekiti wa Wesco Investments Limited, pia ni makamu wa rais wa kampuni ya magari ya Toyota South Africa na Director wa AngloGold. 
 (Stori kutoka,8020fashions.blogspot.com, stori kamili imeandaliwa na Jarida la Forbes)

No comments:

Post a Comment