Tuesday 21 February 2012

MR TWO SUGU NA RUGE MUTAHABA WAPATANISHWA,


Picha:- Waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo Emmanuel Nchimbi, Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (MR II), Meneja uzalishaji vipindi Clouds Media Group Ruge Mutahaba & Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Hatimae Waziri wa habari Emmanuel Nchimbi kwa kushirikiana na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu wamefanikiwa kusuluhisha mgogoro wa kimaslahi kati ya mbunge wa mbeya mjini Joseph Mbilinyi na meneja uzalishaji vipindi CLOUDS MEDIA GROUP Ruge Mutahaba kuhusiana na haki za wasanii wa muziki wa bongofleva.
Waziri Nchimbi amesema “wamekubaliana na kusaini kumaliza tofauti baada ya kufanyika kikao cha mwisho cha upatanishi kati ya Ruge na Mr II ambapo katika upatanishi huo, pande zote mbili ziliridhika kuwa msingi wa mgogoro wao ni kuamini kwamba upande mmoja hauutendei haki upande mwingine”
Waziri Nchimbi amezidi kusema kwamba “kwenye hotuba yangu kwenye bunge lililopita kuhusu vijana Afrika, nilizungumzia haja ya watu kumaliza tofauti zao na kusameheana ambapo baada ya kutoka kwenye mkutano ule Mh Joseph Mbilinyi alikuja kuniona akaniambia muheshimiwa Waziri unajua umeongea mambo ya maana lakini nilitarajia baada ya kusemea pale kwenye kipaza sauti ungekuja kuniambia mimi, haya tuanze huo mchakato wa suluhu, nikamwambia hatujachelewa, bado tunaweza kufanya, nikamuuliza kama ni kweli tufanye mazungumzo ya kuwapatanisha wote wakakubali baada ya kufanya vikao vya kutosha”
Kwa upande wake Ruge Mutahaba amesema “tumepanga mikakati ya jinsi tutakavyokua tunakutana na Mh Sugu kuendelea kusaidia sanaa yetu hii, ni kweli kabisa tumesaini bila shinikizo lolote, tunaamini sasa ni hatua ya kusogea mbele tuachane na yaliyopita”
Mr II alifunga mjadala kwa  kusema  kwamba “ni kweli tulikua katika vita na vita lazima ifike mwisho labda iwe ni vita isiyo na malengo ndio haitaki suluhu lakini kama ilikua na malengo ina maana inapopatikana fursa ya suluhu kama kweli ulikua na dhamira a dhati kwa kile unachokipigania lazima ukubali kukaa chini na kutafuta suluhu ili tusonge mbele, tumekubaliana, sasa tunasonga mbele na wengine sasa hivi tupate fursa sasa hivi kujikita zaidi kwenye siasa za kitaifa”(read more on Millardayo official website)

 Wakati mwingine ugomvi uwa hausaidii,naungana nao kwa hatua waliochukua,Sugu alisisitiza kwa waliokuwa wanaunga mkono ugomvi huu nao waone kuwa sasa yameisha.

2 comments:

  1. i think both are the one who push our music where we are today what we need is 4 them to fight rights of bongo fleva artist coz they ain't get anything i what they do in this industry

    ReplyDelete
  2. uko sahihi,wanamchango mkubwa sana,kugombana sio kitu kizuri

    ReplyDelete