Monday, 12 March 2012

BREAKING NEWS,SALAM ZA TFF KWA YANGA,ADHABU KWA BAADHI YA WACHEZAJI NA FAINI

 
 
 
 
 
 
 
 
 
Polisi akiwazuia wachezaji wa yanga waliokua na hasira na refa.
Refa akikimbia kichapo baada ya kutoa kadi nyekundu nyingine kwa wachezaji wa Yanga ambao mpaka mpira unamalizika, walichapwa 3-1 na AZAM.
Baadhi ya viti vilivyovunjwa.
Baadhi ya mashabiki wa Yanga wanaodaiwa kuhusika na hizo fujo. (picha kutoka kwenye blog ya Dina Ismail - mamapipiro)
Ustaarabu haukuepo kabisa, mashabiki wa Yanga wanadaiwa kukojoa mpaka kwenye sehemu za kunawia mikono.
 
kamati ya mashindano ya TFF imewafungia wachezaji watano wa Yanga kutokana na vurugu zilizotokea hapo siku ya jumamosi kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Azam Fc,
wachezaji waliofungiwa ni Stephano Mwasika aliyefungiwa mwaka mmoja huku Nadir Haroub na Jerry Tegete wakifungiwa jumla ya michezo sita,Nurdin Bakari na Omega Seme wamefungiwa kila mmoja michezo mitatu.
huku Yanga ikipigwa faini ya shilingi milioni 4.5.
habari hii imeandikwa na Shafiidauda.blogspot.com
 
Mi najiuliza mpk sasa kwanini yanga walifanya walichokifanya....!!!!kwani kwenye game si kuna kushindwa pia,mmh!!!

No comments:

Post a Comment