Sunday, 25 March 2012

BWANA SAMWELI TENGA AKIRI KUFANYA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA NA BAADHI YA VIONGOZI WA DIN WAKUBWA NA WANASIASA WAKUBWA,PIA AMEKIRI KUWAONA BAADHI YA WASANII WA MOVIE WA BONGO NA BONGOFLEVA KATIKA JUMBA LA FREEMASON,ALISEMA HAYA AKIHOJIWA NA CLOUDS FM REDIO KUPITIA KIPINDI CHA NJIA PANDA


Japokua anadai alikua mwanachama wa FREEMASONS, Samwel alikua anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya pia na amekiri kufanya biashara hiyo na baadhi ya viongozi wakubwa wa dini wa Tanzania na hata kukaa nao meza moja, hiyo alama kwenye sikio lake la kulia anasema waliwekewa kwa makusudi ili iwe rahisi kutambulika popote atakapotokea, yani ukimuona tu unajua huyu anauza madawa ya kulevya.
 Alama hii ni kubwa ambayo amepigwa katika mguu wake wa kushoto kumtambulisha kuwa ni mwanachama wa FREEMASON, ni alama kama muhuri ambayo imechora ndani ya mfupa ambapo kwa sasa mguu umekuwa ukimuuma sana mpaka kutaka kufanyiwa uparesheni, nembo hiyo baada ya kupigwa iliambatana na KIAPO ambacho popote atakapokwenda atatambulika, alisema kwa sasa ndio inamsumbua sana kwa sababu chuma kilichotumika kumuwekea kimevunja mfupa, na hii aliifanywa huko Afrika Kusini.
---
Bw. Samweli  Tenga ambaye yeye alikwenda nchini Afrika Kusini lakini alikutana na mauza uza mwengi. Alisema kuwa aliamua kukimbilia na kujiondoa kwenye dini hiyo inayodaiwa kuwa ya kishetani baada ya kutoka gerezani huko Afrika Kusini, walikua wanatumwa kwenda kuua watu kwenye ajali na sehemu nyingine, walipewa hirizi maalum za kuwafanya wasioneane lakini baada ya kuona hayawezi hayo maisha alikimbia lakini mpaka sasa anatafutwa kwa sababu alikuwa ndio anamalizia hatua ya mwisho kuingia kwenye  kutajirishwa kwa mali kama inavyotokea kwa waumini wengine, ila akatoroka na baadae ndio akasikia jamaa aliempeleka kwenye hiyo dini nae ameuwawa baada ya kugundulika kwamba alikuwa anataka kujiondoa.
habari hii ni kwa mujibu wa kajunason blog,habari zaidi na kusikiliza clip za mahojiano hayo tafadhali tembelea www.kajunason.blogspot.com,baada ya kusikiliza utaelewa zaidi freemason ni nini!!!!
 

No comments:

Post a Comment