Sunday 25 March 2012

HIVI ITAFIKA MAHALI HII NCHI ITAPUMZIKA KUKOPA?AU YENYEWE KUKOPESHA NCHI NYINGINE?NA WASINGEKUWEPO HAWA WACHINA SIJUI TUNGEKUWA WAGENI WA NANI,!!!!! CHINA NA TZ ZATILIANA SAINI MKOPO NAFUU WA ZAIDI YA 80B KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO

China ni moja ya nchi zizotusaidia sana,tuwashukuru kwa hilo........

Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (kulia ) akisaini kitabu cha wageni cha Wizara ya Fedha jijini  Dar es salaam wakati alipokwenda  kusaini mkopo na misaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali inayozidi shilingi bilioni 80. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(hayupo pichani)  kwa niaba ya Tanzania na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao.
 Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(aliyesimama ) akitoa hotuba jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kusaini mkopo na misaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri Mkulo kwa niaba ya Tanzania na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (hayupo pichani) . Msaada na Mkopo huo unazidi bilioni 80 Fedha za Kitanzania. Kushoto ni Waziri wa Uchukuzi Omar Nundu na kulia ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(kushoto) na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (kulia) wakisaini makubaliano jijini Dar es salaam ya Serikali ya China kuipa mkopo nafuu na msaada kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo nchini. Msaada na mikopo hiyo ni zaidi bilioni 80 fedha za Kitanzania ambayo inazidi kuimarisha urafiki na undugu kati ya Tanzania na China.
Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (aliyesimama ) akitoa hotuba jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kusaini mkopo na misaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya kuisaidia Tanzania. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (hayupo pichani)  kwa niaba ya Tanzania na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao. Kulia ni Balozi wa China nchini Lu Youqing.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliackim Chacha(katikati) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Florence Turuka(kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omar Chambo jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya kusaini makubaliano kati ya Serikali ya China na Tanzania ya kuipa mkopo nafuu na msaada kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo  ambao ni  zaidi bilioni 80 fedha za Kitanzania.(habari na mo-blog)

No comments:

Post a Comment