Tuesday, 6 March 2012

BAADA YA WEMA SEPETU KUVAMIWA NA MWANAMKE ANAEDAI WEMA KAMUIBIA MUME, HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA RAFIKI WA KARIBU WA WEMA, MWIGIZAJI SINTAH

Hii ni moja kati ya picha alizopiga Wema Sepetu alipokwenda kufanya shopping ya dola za kimarekani elfu 40 huko Dubai, shopping ambayo inadaiwa kapelekwa na huyo mume wa mtu.
Leo asubuhi kupitia HEKA HEKA ya LEO TENA CLOUDS FM, alisikika dada mmoja anaedai kuwa mdogo wa mke wa pedeshee mwenye uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu, ambapo yeye ndio anadaiwa kumfanyia Wema Shopping pamoja na kumpa hilo gari jipya aina ya Harrier.
Mwanamke anasema kabla, alikua rafiki mkubwa wa Wema Sepetu na alipoanza kutoka na shemeji yake, alimuonya lakini Wema hakusikia, sasa hata hilo gari Wema analodai kununuliwa na familia kumbe sio kweli, ni la familia ya huyo pedeshee na huwa linatumika kwenye shughuli za kifamilia nyumbani kwake.
Mdogo huyu wa mke wa pedeshee amesema “ni muda mrefu nimegundua anatembea na mume wa dada yangu, ila mwanzo alikua hajui kama ni mume wa dada yangu, nikaja kumwambia akakubali, mpaka ikafikia sehemu akawa hanisalimii… wakati mwingine anaweka nyodo, eti anauliza “eti huyo dada yako ni mzuri kama mimi, kama angekua mzuri si angekua super staa?” sasa jamani hiyo ni akili? eti kaenda dubai kanunua pete ya uchumba anataka huyu mwanaume amvalishe, wakati mwingine Wema anakwenda kwenye pub ya dada yangu yeye na Sintah na wanaume, wanakunywa wanaandika bili mpaka milioni moja na nusu mpaka mbili shemeji ndio analipa, kwa nini asiheshimu hata kama anatembea na mume wa mtu ndo mpaka kwenda kwenye pub ya mke wa mtu?”
Amesema “wakati mwingine anamwambia shemeji yangu ampelekee watoto wake eti akae nao amewamis, hivi jamani hii inaingia akilini? anajua watoto wamepatikanaje hao, eti anataka kuendesha gari la kifahari kama analoendesha mke wa pedeshee….” Wema mwenyewe katumika dunia nzima, hamuingii dada yangu hata robo, amshukuru hata Mungu huyu mtu aliempangia nyumba, kapangiwa Mwananyamala msikitini alafu kijitonyama, namshangaa sana”
kwa mujibu wa Heka Heka ya leo na Gea Habib, mke wa pedeshee huyo amemvamia na kumfanyia fujo Wema Sepetu kutokana na anachokifanya, ambapo Wema alipotafutwa ameomba apigiwe baadae kidogo kwa sababu hayuko sawa kwa sasa.
Mke wa pedeshee huyo kwa kutumia gari lake aina ya Range Rover ameligonga mara tatu kwa hasira hilo gari alilopewa Wema baada ya kumkuta Wema kwenye baa yake (ya mke wa Pedeshee) akinywa pombe na marafiki zake ambapo alijitetea kwamba alikwenda kushoot movie.
hili ndio gari analoendesha Wema Sepetu ambalo inadaiwa ni gari la familia la huyo Pedeshee.
Sasa baada ya hii ishu kutokea, hiki ndio alichokiandika Mwigizaji Sintah kwenye blog yake…

MAONI YANGU:SIJUI ATA KWANINI WEMA HABADILIKI NA HATAKI KUJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA,HABARI HII NIMECHUKUA KUTOKA KWA MILLARD AYO BAADA YA KUONA KILA CHOMBO CHA HABARI  KINAZUNGUMZA KUHUSU WEMA

2 comments: