Kwa mara nyingine tena Lionel Messi anatengeza kichwa cha
habari baada ya kutwajwa kuwa mwanasoka anayelipwa mkwanja mrefu kuliko
wote duniani, huku David Beckham akishika nafasi ya pili na Cristiano
Ronaldo akishika nafasi ya tatu.
Kutokana na ripoti iliyotolewa na jarida la France Football
ambayo imetoka leo, mshambuliaji huyo wa Barcelona anaingiza Pound 33
million kwa mwaka kupitia mishahara na fedha za matangazo wakati LA
Galaxy midfielder na mchezaji wa zamani wa Manchester United David
Beckham ambaye amekuwa akiongoza kwa muda mrefu listi hii, amekuwa wa
pili akiingiza pound milioni 31.5, wakati star wa Real Madrid Ronaldo
akikusanya pound milioni 29.2 ndani ya mwaka mmoja uliopita.
Samuel Eto’o nae yupo katika nafasi ya nne akiingiza pound
milioni 23.3m huku Wayne Rooney akikamata nafasi ya tano na pound
milioni 20.6.

Beckham akiwa mitaani Marekani na watoto wake, kwenye hii picha anaonekana kamkodolea macho yule mrembo pale pembeni....

Hata
kama hajafunga goli kwenye mechi 25 mambo yake ni super sana, nadhani
unamuona hapo ndani ya hicho kitu cheusi cha Aston Martin.

ooOOOOh sijui hafungi magoli sijui nini na nini, akirudi analala hapa..... wewe je? hahah(mmmh millard,eti hafung magoli,ha ha ha ha,uko ndo ulaya)
No comments:
Post a Comment