Tuesday, 13 March 2012

ETI WAKIONGWA MAGARI WANATOA WANAGAWA PENZI KIULAINIIII

I hate those womens who lack self awareness,and those who dont understand their dignity,sikatai kuhongwa ata mimi naweza pewa lakin hawa wadada wenzetu wa Bongooo,noumer sijui ni udaku tu au ndo vile,Society Need changes,
Hawa ni Baadhi ya warembo wanaosemekana wameongwa magari wametoa Utamuu!!!!ila magazeti ya udaku noumer kwani mtu akitoa si wanakuwa wamekubaliana auu?Kwa mfano mi nikiongwa nitakataaa?sijui..........

Wema Isaac Sepetu.

Wolper.HAYA NDO YALIYOANDIKWA NA MWANDISHI WA GAZETI HILI,MMMMHH!!!

SKENDO ya Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu kufumaniwa na gari la familia ya mwanaume anayedaiwa kumhonga ili ‘kujilia vyake kiulaini’, imeibua tafsiri kuwa mastaa wa kike wengi wanaumwa pepo la gari.
Uwazi, lina orodha ya mastaa wa kike ambao kwa nyakati tofauti, walikumbwa na taadhira ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria baada ya kutaka kufanya ujanja ili wayamiliki jumla magari waliyodaiwa kuhongwa.
KUHUSU WEMA
Mrembo huyo ambaye hivi sasa amejikita kwenye ulimwengu wa filamu, Jumapili ya Machi 4, 2012, aliponea chupuchupu baada ya kuvamiwa na mwanamke aliyetajwa kwamba ni mtumishi wa Ikulu.
Wema alivamiwa nje ya Pub ya Last Drop iliyopo Mwanamboka, Kinondoni, Dar es Salaam, huku mwanamke aliyefanya uvamizi huo akitaja sababu kuwa gari aina ya Lexus analoendesha mrembo huyo ni mali ya familia yake na anao ushahidi kwamba alihongwa na mume wake.
NI AIBU YA WENGI
Staa wa filamu, Jacqueline Wolper, ana rekodi ya kudhalilishwa na gari alilodaiwa kuhongwa na boyfriend wake wa zamani, Exaud Macha.
Wolper, alikabidhiwa gari aina ya Toyota Cresta GX 100 bila kadi, hivyo mapenzi yalivyokwisha Macha alitaka ‘mkoko’ wake urudi kwenye himaya yake.
Hata hivyo, mrembo huyo aling’ang’ania gari hilo, hivyo kulifanya shauri hilo kutinga polisi.
Katika utetezi wake, Wolper alidai kwamba Macha ni mjomba wake na alitaka kumbaka, madai ambayo jamaa huyo aliyakana na kubainisha jinsi uhusiano wao ulivyoanza mpaka ukafa.
Staa mwingine wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’, alikumbwa na ‘mtiti’ wa gari aina ya Toyota Carina alilodaiwa kuhongwa na aliyekuwa boyfriend wake, Donald Mwakamele ‘McDonald’.
Mapenzi ya Johari na McDonald yalipokufa, mrembo huyo alibaki na gari hilo, hivyo kuibua kesi iliyofika kwenye vyombo vya sheria.
Johari alidai gari hilo alipewa na McDonald kwa mapenzi yake baada ya kukolea kwake, wakati jamaa huyo aliporomosha tuhuma kwamba mrembo huyo alimuibia.

NI UGONJWA MKUBWA
Kwa mujibu wa staa wa filamu (jina tunalo), mastaa wa kike wataendelea kudhalilishwa na wanaume wenye fedha kwa sababu wana tamaa ya magari.
“Tunafanya nao kazi, tunaona matarajio yao. Tamaa ndiyo inawaponza. Wengi wanatoa mapenzi hovyo kwa ahadi za kununuliwa magari, wengine wanapewa bila kadi, wakitibua wananyang’anywa.
“Nashauri kila mmoja akajituma kwenye eneo lake, watafute fedha na wanunue magari kwa nguvu zao wenyewe. Siyo kila siku kutegemea wanaume, wataendelea kutumiwa na kuchezewa kila siku,” alisema staa huyo huku akisisitiza jina lake lisitokee gazetini.

1 comment:

  1. mmezidi tamaa bila magari hamuwezi kuwa mastaa kwani ustaa ni kudrive na si vinginevyo dunia na karne ya sasa tuliyonayo utapeli kila kona mapenzi nayo siku hizi yameingiliwa wadada wamezidi kuwa na tamaa ndiyo maana wanaume wengi wanapata advintage ya kutushawishi ukimwona mwanaume anadrive utamtolea macho basi hata akikujaribu tu ni kosa la jinai hata magari ya kuazima siku hizi watu wanatumia kwa kutongozea si hujui chochote unachojua kila umwonae anadrive unajua la kwake tutamalizwa jamani tuwe makini.

    ReplyDelete